Ripoti ya Afisa Mkuu Mtendaji Wa Shirika
Mwaka wa 2020 utakumbukwa kama mwaka ambao kwa hakika haukutarajiwa kuwa kama ulivyokuwa huku tandavu ya Covid-19 ikishambulia mataifa yote ulimwenguni. Tandavu hii ilikuwa sio tu janga la kiafya - athari zake ziligusa nyanja za kiuchumi na kijamii pia – huku uchumi wa mataifa mbalimbali barani Afrika ukiachwa katika hali ya hatari kutokana na kupungua kwa shughuli za ndani ya nchi hizo pamoja na vikwazo vya usafiri na biashara ambavyo hatimaye vilikuja kuwa hali ya kawaida mwaka wa 2020. Mashirika kama Umoja wa Afrika na IMF yalitabiri kwamba ukuaji wa GDP ya bara hili ungepungua kwa -0.8% kutoka kwa ubashiri wa awali wa 3.2% kutokana na tandavu hii. Utafiti wa Benki ya Dunia uliofanywa 2020 ulionyesha kwamba biashara katika sekta za kibinafsi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki zilikabiliwa na kupungua kwa hitaji la bidhaa na huduma kutokana na kupungua kwa matumizi, kuvurugwa kwa mikondo ya usambazaji bidhaa, uwezo wa kufikia bidhaa, mikondo ya leba na mauzo kutokana na tandavu hii.
Changamoto hizi zikawa kubwa hata zaidi kutokana na vikwazo vilivyowekwa na serikali za ukanda huu ili kuzuia viwango vya maambukizi kutoka nchi moja hadi nyingine. Athari hii kwenye sekta ya kibinafsi na kampuni za ndani ya nchi zilifika chini hadi kwa familia kupitia kupunguzwa kwa saa za kufanya kazi, kukatwa kwa mishahara na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, na hivyo kupunguza uwezo wa watumiaji kununua bidhaa.
Download Full CEO's Statement